Nyumba ya dola 700

Kampuni ya Tata ya India inasema itaanza kujenga nyumba rahisi, ili kuwasaidia watu maskini kumudu kununua nyumba - nyumba ambazo kuta zake tayari zinatengenezwa kiwandani.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Msemaji wa Tata, kampuni ambayo miaka miwili iliyopita ilianza kutengeneza gari rahisi kabisa duniani, liitwalo Tata Nano, alieleza kuwa nyumba hizo zinaanza kujaribiwa kujengwa sehemu mbali mbali za India.

Alisema nyumba hizo zitakuwa tayari mwakani, na zitagharimu dola 700 tu.

Wakuu wa India wanasema nyumba milioni 15 zinahitajika mashambani.