AU inapendekeza mkutano kuhusu Libya

Wapiganaji wa Libya wamekaribisha pendekezo la Umoja wa Afrika kuanza mazungumzo, bila ya kumshirikisha Kanali Gaddafi moja kwa moja.

Haki miliki ya picha Reuters

Penedekezo hilo la kuzungumza mustakbali wa Libya, lilitangazwa katika taarifa iliyotolewa mwisho wa mkutano wa viongozi wa AU uliofanywa Equatorial Guinea.

Msemaji wa wapiganaji wa Libya alieleza pendekezo hilo kuwa hatua kubwa na alisema inaonesha Kanali Gaddafi hatokuwamo katika mustakbali wa Libya.

Taarifa ya AU piya ilitoa wito kuwa mapigano yasitishwe na kuwe na kipindi cha mpito, kitachoelekeza nchi kwenye uchaguzi wa kidemokrasi.