Jeshi la Nigeria linakosolewa

Gavana wa jimbo la Nigeria ambako kulitokea fujo karibuni, inayotokana na kikundi cha kiislamu cha Boko Haram -- amekiri kuwa jeshi lilitumia nguvu za kukithiri.

Kashim Shettima, gavana wa jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria, aliiambia BBC kwamba wale ambao nyumba na magari yao yaliangamizwa, watalipwa fidia.

Piya aliwaambia watu waliohama maeneo yao, warudi nyumbani.

Mashirika ya haki za kibinaadamu yamelishutumu jeshi la Nigeria kwamba liliuwa watu kiholela, wakati wa kupambana na Boko Haram.