Rushwa inazidi Afrika Kusini

Chama kikuu cha wafanyakazi cha Afrika Kusini, kimeonya kuwa rushwa nchini imezidi, na imefikia kiwango cha kuweza kuigeuza nchi hiyo, kuwa nchi isiyokuwa na nidhamu.

Msemaji wa Jumuiya ya wafanyakazi, COSATU, alisema madai ya ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma yanazidi kuongezeka.

Wakati huo huo mashirika mengine, ambayo yanamuunga mkono Rais Jacob Zuma, yalipokea vema uamuzi wa serikali, wa kuanzisha uchunguzi kuhusu tuhuma za ufisadi ndani ya jeshi la polisi.

Msemaji wa COSATU, Patrick Cravan, alisema swala hilo lazima lipewe uzito na wakuu:

"Ikiwa hatuchukui hatua kali dhidi ya vitendo hivi, basi tutafikia hali ambapo wahalifu wataweza kuiba mali ya taifa watakavyo, bila ya kufikishwa mahakamani."