Ban Ki-moon anasihi ushirikiano Sudan

Kati ya wageni mashuhuri wa kimataifa waliohudhuria ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bank Ki-moon, ambaye alizisihi nchi mbili zilizoundwa leo zishirikiane.

Haki miliki ya picha AFP

"Sudan Kusini imara itaihitaji Sudan Kaskazini.

Na vivyo Kaskazini itahitaji Kusini.

Leo ni siku yao, Kaskazini na Kusini, kuthibitisha historia yao na kutegemeana.

Ni nafasi ya kuthibitisha tena ahadi ya kujenga uhusiano wa amani, wenye manufaa, na kukabili hatima yao kama washirika - siyo washindani"

Rais Bashir wa Sudan Kaskazini amehudhuria sherehe hizo, na serikali yake imemtambua jirani yake mpya, lakini bado kuna mizozo kati yao, ambayo inaweza kuzusha mapigano.

Serikali ya Khartoum imethibitisha kuwa waSudan Kusini hawatokuwa tena raia wa kaskazini, na mipaka baina ya nchi mbili hizo bado haijakubaliwa.

Piya pande hizo mbili hazijafikia muafaka juu ya namna ya kugawana mafuta, na mapigano yamezuka katika maeneo ya mpaka baina yao.

Umoja wa Mataifa umeunda kikosi kipya kwa ajili ya Sudan Kusini, cha kusaidia kuimarisha amani.