Senegal isimrejeshe Habre Chad

Hissene Habre atakabiliwa na hukumu ya kifo iwapo atarejeshwa nchini Chad.

Haki miliki ya picha
Image caption Hissene Habre

Kamishna wa Shirika la kutetea haki za binadaamu la Umoja wa Mataifa ameihimiza serikali ya Senegal kutotekeleza mipango yake ya kumrejesha nyumbani aliyekuwa rais wa Cad, Hissene Habre, ambako atakabiliwa na hukumu ya kifo, iliyotolewa akiwa ng'ambo.

Navi Pillay alieleza wasiwasi wake kuwa Bw Habre huenda akateswa nchini Cahd.

Siku ya Ijumaa serikali ya Senegal ilisema Bw Habre atasafirishwa kwa ndege na kuwasili Chad tarehe 11 Julai.

Bw Habre anashutumiwa kwa kutekeleza mauaji na utesaji ya maelefu ya wapinzani wake kati ya miaka ya 1982 na 1990, shutuma ambazo amekanusha.

Mkandamizaji

Bi Pillay Jumapili alisema "Naihimiza serikali ya Senegal itazame upya uamuzi wake."

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Navi Pillay

"Kama mwanachama wa Makubaliano ya Kupinga Utesaji (Convention Against Torture), Sengal haikubaliwi kumuondoa mtu nchini ikwa kuna wasiwasi ya kumweka mtu huyo hatarini ya kukabiliwa na utesaji."

Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu pia yameelezea wasiwasi wao kuhusu uamuzi wa Senegal yakisema kuwa Bw Habre hatapata haki nchini Chad.

Bw Habre amekuwa akiishi katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, tangu alipoondolewa madarakni mwaka 1990.

Mwaka 1992 tume ya ukweli nchini Chad ilimshutumu kwa kuhusika na utesaji na mauaji ya watu arobaini elfu alipokuwa kiongozi kwa miaka minane.

Mwaka 2008 alihukumiwa kifo akiwa ng'ambo kwa mashtaka ya kupanga kuipindua serikali.

Senegal ilimkamata Bw Habre mwaka 2005 baada ya kushtakiwa na Belgium kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na utesaji.

Belgium pia imekuwa ikiiagiza Mahakama ua uhalifu wa kivita, ICC, kumpeleka Bw Habre Belgium ili akabiliwe na kesi dhidi yake.