Kumi wauawa kaskazini mwa Nigeria

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mji wa Maiduguri, Nigeria Kaskazini

Takriban watu 10 wameuawa katika msururu wa mashambulio yanayohusishwa na kundi la wapiganaji wa kiislamu katika mji wa kaskazini mashariki wa Maiduguri,maafisa wanasema.

Watu waliokuwa na bunduki siku ya Jumamosi waliwapiga risasi watu wanne na mtu mmoja siku ya Jumapili.

Image caption Kundi la Boko Haram lazidisha mashambulio

Jenerali Nwaogbo alilaumu kundi la Boko Haram kwa mauaji hayo, ambalo linataka kuwa na jimbo linalotawaliwa kwa sheria za kiislamu kaskazini mwa Nigeria.

Kundi hilo pia limelaumiwa kwa kushambulia eneo lengine la burudani katika mji huo huo siku ya Jumapili iliopita na kuwaua watu 25.

'Matukio hatari '

Bomu la siku ya Jumapili lililipuka katika klabu cha pombe karibu na kambi ya polisi katika eneo la Wulari huko Maiduguri,alisema Jenerali Nwaogbo,mkuu wa jopokazi la pamoja la polisi na wanajeshi.

Maafisa wanasema watu watano waliuawa.Jenerali Nwaogbo ameambia shirika la habari la AFP kuwa watu wanane walifariki dunia,huku afisa mwengine akitaja idadi ya waliouawa kuwa 10.

Mkaazi wa eneo hilo anasema alisikia mlipuko, na baadaye akaona moshi mweusi ukitanda juu ya klabu hicho cha pombe.