Wahamiaji 197 wazama Sudan

Takriban watu 200 wamefariki dunia katika bahari ya sham wakati boti lilokuwa limebeba wahamiaji haramu kuelekea Saudia Arabia lilipozama katika pwani ya Sudan, shirika la habari la Sudan linasema.

Image caption Bahari ya Sham

Kituo cha habari cha Sudan,kinachofahamika kuwa na uhusiano wa karibu na serikali ya nchi hio,kinasema kuwa watu watatu pekee walinusurika.

Boti liliwaka moto,na ndani kulikuwa na watu waliokuwa wanataka kuingia Saudi Arabia kutumia njia haramu, shirika hilo lilisema katika taarifa yake.

Wanasema wahamiaji hao walikuwa wanatoka nchi zinazopakana na Sudan. Haijafahamika pale walipoanzia safari yao.

Mwandishi wa BBC mjini Khartoum James Copnal anasema bahari ya sham ni njia inayofahamika kupitisha wahamiaji haramu wanaokwenda Saudi Arabia na Yemen.