Nana Rawling wa Ghana ashindwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bi Nana Rawlings

Mke wa aliyekuwa kiongozi wa Ghana Jerry Rawlings ameshindwa katika juhudi zake za kuwania urais kupitia chama chake kwenye uchaguzi wa mwaka ujao.

Nana Konadu Rawlings alishinda kwa asilimia 3.1 tu ya kura zote, katika mkutano wa chama cha National Democratic Congress (NDC) kwenye mji mkuu, Accra.

Chama hicho kimeidhinisha Rais John Atta Mills ndiye agombee.

Wachambuzi wamesema kugombea kwa Bi Rawlings kumeonyesha nia ya mumewe ya kuwa na ushawishi zaidi katika chama hicho.

Mwandishi wa BBC David Amanor mjini Accra alisema Bi Rawlings aliondoka haraka kwenye ukumbi wa mkutano baada ya kushindwa.

Mwandishi wetu alisema, wafuasi wake wameilaumu tume maalum ya uchaguzi na baadhi ya viongozi wa kike kwa kushindwa kwake.

Wakati wa kamepni, Bi Nana alisema alikuwa akimpa changamoto Bw Atta Mills "kuiokoa" NDC.