Murdoch aondoa ombi la umiliki

Akitumia fursa iliyochagizwa na mtiririko wa madai kuhusu udukuzi kupitia simu David Cameron amesema kuwa anafahamu ni kiwango gani cha ghadhabu kilichosababishwa na kashfa ya udukuzi na kwamba wahusika lazima wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

Image caption Wazir Mkuu

Amesema kuw awakati umewadia kwa Jaji kuchunguza malipo yaliyotolewa na wandishi habari wa gazeti la News of the World kwa polisi.

Jaji huyo, akaongezea, atakuwa na mamlaka ya kumhoji mwandishi, mmiliki wa gazeti, wanasiasa na maofisa wa polisi.

Amesema kuwa tume hiyo pia itachunguza usimamizi wa sheria ya vyombo vya habari vya hapa Uingereza. Ingawaje hili limeonyesha kama David Cameron alitawala mjadala bungeni leo bado anakabiliwa na shinikizo kuhusu kashfa hiyo.

Wabunge wanatazamiwa kujadili athari zilizosababishwa na vitendo vya kihalifu vilivyoko kwenye magazeti yanayoendeshwa na kampuni ya Bw.Murdoch ya News International. Na kupitia kura, vyama vyote vikuu vitatu vinatarajiwa kupinga na kuteka mpango wa mmiliki huyo wa vyombo vya habari wa kumiliki chombo muhimu cha runinga cha B SKY B.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Shirika la utangazaji

Wakati akizongwa na kashfa ya udukuzi wa simu haikudhaniwa kama ombi lake la kutaka kampuni yake ya News International imiliki shirika la utangazaji la B SKY B utakubalika.

Habari hizi zimetoka saa mbili baada ya Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kujibu vikali kashfa hio, akimtaka mmiliki Rupert Murdoch asiendelee kufikiria jinsi ya kufanikisha ombi lake la kumiliki kikamilifu shirika la utangazaji la BSkyB na kwamba badala yake atulize kampuni yake.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Magazeti ya Murdoch
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rupert Murdoch

Hili ni pigo kubwa kwa Bw.Murdoch na aibu kwa mtu ambaye kwa mda mrefu wanasiasa wamekuwa wakimuenzi na kwa sasa ni mabadiliko ya majaliwa ya mmojapo wa watu mashuhuri na wenye ushawishi duniani.

Ingawa ombi hilo linaweza likarejelewa siku za baadaye, uwamuzi wa kuliondoa ombi hilo hivi sasa litaiathiri kampuni ya News Corp kiasi cha makumi ya mamilioni ya dola za Kimarekani.