Shambulio la maguruneti Rwanda

Mlipuko wa guruteni uliotokea kusini magharibi mwa mji wa Kamembe nchini Rwanda, umesababisha majeruhi ishirini na moja.

Hili ndio shambulio la hivi karibuni katika msururu wa mashambulizi yaliyoanza mwaka jana na ambayo kufikia sasa yamesababisha vifo vya watu kumi na kujeruhi wengine wengi.

Mji huo unapakana na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Serikali ya Rwanda imekuwa ikilaumu kundi la waasi wa FDLR pamoja na wapinzani wa serikali kama wanaofanya mashambulizi hayo.