Misri yatangaza baraza jipya la Mawaziri

Baraza jipya la Mawaziri limeapisha nchini Misri, huku maandamano ya kuipinga serikali yakiendelea. Zaidi ya nusu ya mawaziri wamebadilishwa, ingawa Waziri Mkuu, Essam Sharaf, anaendelea kubakia katika wadhifa wake.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Baraza tawala la Misri

Hadi kufikia uwamuazi wa kuunda serikali mpya ya Misri kumekuwepo na vigezo na matatizo pia. Uteuzi wa baraza jipya la Mawaziri ulicheleweshwa mwanzoni kutokana na mabishano baina ya Waziri mkuu na baraza la kijeshi linalotawala, kisha Waziri mkuu akapelekwa hospitali kwa sababu ya shinikizo la damu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Essam Sharif

Kisha baraza likabadilishwa, hadi wakati wa kula viapo walipoapishwa na kiongozi wa kijeshi Field Marshal Tantawi.

Mabadiliko hayo hayajafanikiwa kikamilifu, katika nia yake ya kuwaridhisha upinzani ingawa yameweza kupunguza makali ya waandamanaji waliokwama katika medani ya Tahrir.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption medani ya Tahrir-Misri

Wakati baraza jipya likiiapishwa, koto moja mjini Cairo ikaondoa amri kwamba jina la aliyekuwa Rais, Hosni Mubarak liondolewe kutoka majengo yote ya umma. Uwamuzi huu ulisababisha malumbano baina ya waungaji mkono na wanaompinga kiongozi aliyeondoka madarakani nje ya majengo ya mahakama.