Kenya kufungua kambi ya Ifo II

Waziri Mkuu Raila Odinga Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri Mkuu Raila Odinga

Serikali ya Kenya imeamuru kufunguliwa kwa kambi ya Ifo kaskazini mashariki mwa Kenya ambako maelfu ya watu wanawasili kila siku wakikimbia ukame na mzozo nchini Somali.

Amri hii imetolewa na Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga aliyetembelea kambi ya wakimbizi ya Dadaab ambayo ni kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani , ikiwahifadhi wakimbizi zaidi ya elfu mia tatu na mia nane, idadi ambayo ni kubwa kuliko uwezo wa kambi hiyo.

Serikali ya Kenya ilikuwa imekabiliwa na shinikizo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kufungua kambi nyingine lakini ikawa na hofu juu ya usalama wa nchi na kuhofia kwa wakimbizi hao wakejenga makao ya kudumu nchini Kenya.