Rais Obama atofautiana na upinzani.

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Barack Obama

Rais Barack Obama amekuwa na kikao kilichokumbwa na mjala na maneno makali wakati wa kujadili nakisi ya bajeti ya kitaifa.

Mmoja wa wabunge wa upinzani aliyeshiriki kikao hicho ambacho kilikuwa cha nne na kushirikisha wabunge wa upinzani kutoka chama cha republican amenukuliwa akisema kwamba rais Obama alionekana mwenye kero na kuapa kutoridhia masharti ya upinzani na liwalo liwe.

Hata hivyo mmoja wa wabunge wa Democrats amesema taarifa kwamba rais aliondoka kwa ghathabu kutoka kikao hicho zilitiliwa chumvi.

Awali mmoja ya mashirika ya kutathmini viwango vya uchumi wa dunia ilionya dhidi ya uchumi wa Marekani kudorora zaidi ikiwa taifa halitatua nakisi ya bajeti inayokisiwa kufikia dola trilioni 14.