Aliyekuwa mkuu wa majeshi akamatwa

Aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Guinea amekamatwa kufuatia shambulio lililofanyika nyumbani kwa Rais Alpha Conde kwenye mji mkuu, Conakry.

Mke wa Jenerali Nouhou Thiam alisema mume wake alichukuliwa saa chache baada ya shambulio hilo.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais Alpha Conde

Bw Conde ambaye alikuwa nyumbani kwa wakati huo ametoa wito wa kuwepo na utulivu.

Takriban mtu mmoja amefariki dunia.

Sehemu kadhaa za makazi ya rais ziliharibiwa baada ya kushambuliwa na silaha kali mapema Jumanne asubuhi.

Bw Conde aliingia madarakani katika uchaguzi uliofanyika Desemba iliyopita, baada ya utawala wa kijeshi uliodumu miaka miwili nchini humo.