Mmarekani akiri kuhusika na shambulio

Haki miliki ya picha AP
Image caption Al-Shabab

Mtu mmoja kutoka jimbo la Minnesota nchini Marekani amekiri kuwasaidia watu wenye asili ya Kisomali kusafiri kwenda Afrika kuungana na kundi la wapiganaji la al-Shabab.

Omer Abdi Mohamed amekiri mashtaka ya kufanya jaribio la mauaji na utekaji nyara katika nchi ya kigeni.

Kukiri kwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 kumetokea siku ambayo ingetakiwa kuwa kesi ya mwanzo kufanywa na serikali ya Marekani inayohusu kuajiriwa kwa wapiganaji wa Kimarekani kwa ajili ya al-Shabab.

Mohamed anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 gerezani atakapohukumiwa baadae.

Wakili wake, Peter Wold, alisema Mohamed aliamua kukiri makosa ya kusaidia kwa kutoa vifaa kwa magaidi kwasababu ana familia na atakabiliwa na miaka mingi zaidi akikutwa na hatia.