Umuhimu wa Lower Shabeelle katika kilimo

Eneo la Lower Shabeelle ndilo lenye watu wengi zaidi katika maeneo kumi na nane ya utawala nchini Somalia. Wakulima katika eneo hilo wamebarikiwa na ardhi yenye rotuba na maji kutoka mto Shabeelle ambao ndio chanzo cha maji muhimu katika eneo hilo.

Image caption Kupunga kwa uazlishaji wa vyakula katika eneo la shabelle kumechangia tatizo hili la njaa

Huko ndipo chakula ambacho hutumika katika maeneo yote ya somalia kinazalishwa. Katika siku zilizopita, wakulima katika eneo hili waliokuwa wanakuza ndizi walikuwa wakiziuza katika soko za nchi za bara la Uropa.

Wanyama wengi kama vile ng'ombe na angamia wanafugwa hapa na kuwapa wakazi nyama na maziwa.

Miji ya Lower Shabeelle ni pamoja na Jannale, ambayo maana yake ni mbinguni. Mji huo ulipewa jina jino kwa sababu ya ardhi yake ambayo haijakauka, mashamba makubwa , maji mengi na pia kwa sababu inakaribia ukingo wa bahari ujulikanao kama Sambusi ambapo viumbe vya kipekee vya baharini ambavyo hutumika kama kituweo hupatikana.

Kufeli kwa msimu wa mvua kumechangia janga linaloathiri watu wa Somalia , lakini pia hali hii imechochewa na miaka mingi ya vita.

Tangu kusambaratika kwa serikali ya Somalia miaka ishirini iliyopita, wababe wa kivita wamekuwa wakipigania utawala wa eneo la Shabeelle ya chini. Katika hali hii wakulima wameteswa na wapiganaji hao na miradi ya kilimo ya unyunyuzaji wa maji imeathirika.

Kwa muda wa miaka mitatu iliyopita, eneo hilo limekuwa chini ya utawala wa kundi la wapiganaji wa Al Shabaab . Ingawa watu wanasema kumekuwa na amani katika eneo hilo kwa sababu ya utawala huo, uzoefu wao wa kupiga watu mijeledi umefanya wengi waondoke kutoka eneo hilo.

Wasomali wengi, ikiwa ni pamoja na watu wenye ustadi katika kazi zao, na ambao wamehamia Kenya, wanatoka eneo hilo.

Ukame ulioko Somalia kwa sasa umeathiri maeneo yote ya Somalia kwa sababu kiwango cha chakula ambacho kilikuwa kinakuzwa huko Lower Shabeelle kimepungua na pia idadi kubwa ya wakazi wa eneo hilo wamehama.