Huwezi kusikiliza tena

Umeme Tanzania bado kitendawili

Tanzania ni moja ya nchi za Afrika Mashariki ambayo kwa muda mrefu sasa imekuwa ikikabiliwa na tatizo sugu la umeme.

Maelezo yanayotolewa na serikali ya Tanzania pamoja na shirika la Umeme Tanzania Tanesco ni kuwa ukame ndio chanzo kikuu cha matatizo ya umeme nchini humo.

Kwa nchi za Afrika Mashariki Tanzania ndio inayoongoza kwa kukumbwa na uhaba wa umeme mara kwa mara, licha ya kuwa nchi nyingine za Jumuiya hiyo kama Burundi na Uganda zimekuwa zikikabiliwa na upungufu wa umeme.

Katika mjadala wa kila leo, tunaangazia tatizo la umeme hasa kwa Tanzania, athari za ukosefu wa umeme kwa Tanzania yenyewe na pia nchi nyingine za Afrika Mashariki kiuchumi.

Washiriki ni James Shikwati, mchambuzi wa mausala ya Uchumi kutoka Kenya, Bi. Badra Masoud, Afisa Uhusiano kutoka Shirika la Umeme Tanzania TANESCO na Hassan Mhelela Mwandishi wa BBC aliyeko Dar es salaam, ambaye ndio ametoka tu kutembelea bwawa la Mtera lililoko mpakani mwa mkoa wa Dodoma na Iringa.

Mjadala umeendeshwa na Zawadi Machibya.