Usalama Iraq umepungua

Shirika la Marekani linaloshughulika na ukarabati wa Iraq, linasema hatari imezidi nchini humo kushinda mwaka jana.

Mkuu wa Ukarabati wa Iraq, Stuart W Bowen Junior, alisema mauaji ya wanajeshi wa Marekani na watu maarufu wa Iraq, pamoja na miripuko ya mabomu na mashambulio katika eneo la salama, liitwalo Green Zone, mjini Baghdad, yamezidi hivi karibuni.

Lakini bado hayakufikia kiwango cha wakati wa kilele cha fujo nchini Iraq.

Alisema kuwa jeshi la Marekani linadharau fujo hizo zinazoendelea, miezi michache tu kabla wanajeshi kuondoshwa nchini humo.