Mutharika ateua kamanda mpya

Rais Bingu wa Mutharika wa Malawi amemteua mkuu mpya wa jeshi, siku mbili baada ya waandamanaji 18 kuuwawa, pale polisi walipofyatua risasi na moshi wa kutoza machozi, ili kuzima maandamano sehemu mbali mbali za nchi.

Haki miliki ya picha AP

Brigadier-Jenerali Henry Odillo amechukua nafasi ya Jenerali Marko Chiziko, ambaye mkataba wake wa ajira umemalizika.

Nchi sasa ni shuari lakini viongozi wa maandamano, wameonya kuwa watafanya maandamano mengine iwapo rais hatozungumza nao.