Breivik alilenga kwengine piya

Polisi wa Norway wamethibitisha kuwa Anders Behring Breivik, ambaye amekiri kuuwa watu 76 juma lilopita, alikuwa akifikiria malengo mengine piya.

Haki miliki ya picha Reuters

Watu 69 waliuwawa katika kisiwa cha Utoeya, na 8 kwenye mripuko wa bomu lilotegwa kwenye gari, kati ya mji wa Oslo, mapema siku hiyo hiyo.

Msemaji wa polisi, Paal-Fredrik Hjort Kraby, alieleza kuwa alipohojiwa, Breivik alizungumza kwa jumla kwamba alikuwa na malengo mengine piya.

Lakini msemaji huyo alikataa kuthibitisha tetesi kwenye vyombo vya habari kwamba kati ya malengo hayo, ni kasri ya kifalme na makao makuu ya chama tawala cha Labour.