Meli yatekwa Afrika Magharibi

Haramia Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Haramia

Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Utaliana imesema kuwa meli ya kubeba mafuta ya Utaliana, imetekwa na maharamia Afrika Magharibi, karibu na Ghuba ya Guinea.

Maharamia watatu walipanda katika meli hiyo, kusini ya mti wa Cotonou, mji wa biashara wa Benin, leo alfajiri.

Uharamia mara nyingi unatokea Afrika Mashariki, lakini Afrika Magharibi ni nadra.