Ndege ya Kijeshi yapata ajali Morocco

Image caption Morocco

Ndege ya kijeshi imeanguka kusini mwa Morocco, taarifa rasmi kutoka Shirika la habari la MAP na afisa mmoja zimesema.

MAP halikutoa taarifa ya idadi ya abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo ya jeshi aina ya C-130 Hercules lakini ajali hiyo imetokea katika eneo la Guelmine, kaskazini mwa eneo lenye mzozo la ngome ya Western Sahara.

Afisa mmoja wa Wizara ya Mambo ya Ndani aliliambia Shirika la Habari la AFP watu kadhaa wamekufa.

"Hii ni ndege ya kivita inayotumika kusafirisha wanajeshi, lakini pia familia zao," afisa huyo alisema.

Alisema ilikuwa inatumika zaidi katika Sahara.

"Pamoja na hayo, ilikuwa ni ukungu na hali mbaya ya hewa ndio vinaaminika kuwa chanzo cha ajali. Lakini kwa sasa hatuna taarifa za kamili," afisa huyo aliiambia AFP.