Wigan yaafiki ada ya Villa kwa N'zogbia

Aston Villa imeafikiana na Wigan Athletic ada ya kumsajili winga hatari Charles N'Zogbia.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Charles N'Zogbia

N'zogbia raia wa Ufaransa mwenye wa umri wa miaka 25, kwa sasa anajiandaa kuzungumzia marupurupu yake binasfi na klabu ya Aston Villa.

Klabu ya Aston Villa imesema wanamatumaini ya kukamilisha kila kitu wakijijenga upya baada ya kuwauza Stewart Downing na Ashley Young.

Klabu zote hizo mbili hazijatangaza ada waliyoafikiana, ingawa taarifa nyingine zinasema ni kiasi cha paundi milioni 9.5.

Meneja wa Aston Villa Alex McLeish msimu uliopita nusura afanikiwe kumsajili N'Zogbia wakati akiifundisha Birmingham City, ingawa mipango ikashindikana kutokana na mahitaji binafsi ya N'zogbia.