Huwezi kusikiliza tena

Shambulio baya kutokea Norway

Mwishoni mwa wiki iliyopita kulitokea shambulio kubwa la bomu nchini Norway na baada ya saa moja mtu aliyekuwa na bunduki aliwaua vijana wengi waliokuwa mkutanoni katika kisiwa cha Utoya. Mtu huyo Anders Behring Breivik, alikiri kufanya mashambulio yote mawili na tayari amefikishwa mahakamani.

Breivik katika maelezo yake alisema alifanya mashambulio hayo kwa sababu ya kuchukizwa na nchi yake pamoja na nchi nyingine za Ulaya kukumbatia wageni na pia kwa mtazamo wake Ulaya inatekwa na Uislamu.

Walioshiriki kwenye mjadala huu ni

1) Dr Yusuf Saleh Salim- mchambuzi anayeishi nchini Denmark kwa miaka mingi akiwa na uzoefu wa nchi hizo zilizo jirani na Norway

2) Maggid Mjengwa- mwandishi wa habari wa Tanzania/Mwalimu na amekaa zaidi ya miaka 10 Sweden na kwa sasa yupo nchini humo.

3) Sven Olsen- mkazi wa Norway, raia wa huko na anazungumza Kiswahili

4) Muhammed Semboja- mkaazi wa Norway, Oslo.

Aliyeongoza mjadala huu ni Charles Hilary.