Sherehe za mwaka mmoja kabla ya Olimpiki

Sherehe zinafanyika jijini London kuadhimisha mwaka mmoja kamili kabla ya kuanza michezo ya Olimpiki ya mwaka 2012.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mwaka mmoja kabvla kuanza Olimpiki

Kituo cha kuogelea katika Olympic Park , Stratford kitazinduliwa na anaetarajiwa kushinda medali ya Olimpiki Tom Daley akiwa mchezaji wa kwanza kupiga mbizi.

Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olympiki (IOC) Jacques Rogge atakua katika uwanja wa Trafalgar Square ambako mifano ya medali zitakazokua zikitolewa katika michezo hiyo zitazinduliwa.

Mwenyekiti wa Kamarti ya matayarisho ya Olimpiki 2012 Lord Coe amesema mipango yote imekwenda kama ilivyopangwa.

Amesema hii ni siku kubwa kwa kamati ya matayarisho akiongeza kuwa wamepokea maombi millioni 23 ya tiketi kutoka watu milioni mbili na kwamba watu laki mbili na elfu 50 wamejitolea kutumika wakati wa michezo hii.

Katika sherehe za Trafalgar Square, usiku Bwana Rogge na Meya wa jiji la London, Boris Johnson wataialika dunia kuja London kusherehekea michezo hii majira ya kiangazi mwakani.

Bendi ya muziki wa Pop, The Feeling, kwaya za nyimbo za dini na na DJ wa Radio 1 DJ Kissey Sell Out ni miongoni mwa watakaotumbuiza.