Bahrami amsamehe aliyempofua

Ameneh Bahrami Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ameneh Bahrami

Mwanamke wa Iran ambaye alipofoka aliposhambuliwa kwa tindi kali, amemsamehe mwanamme aliyemshambulia, saa chache tu kabla ya mfungwa huyo akitarajiwa naye kupofolewa, kama adhabu yake.

Majid Movahedi alikutikana na makosa ya kumrushia tindi kali usoni Ameneh Bahrami, baada ya bibi huyo kukataa posa yake mara kadha.

Baada ya hukumu kutolewa, Ameneh Bahrami alisema yeye mwenyewe atamimina tindi kali kwenye macho ya Bwana Movahed. Mashirika ya kupigania haki za kibinaadamu yalilalamika juu ya hukumu hiyo.

Bi Bahrami sasa ameliambia shirika la habari la Iran, kwamba, ingawa Mungu anataja adhabu ya malipo, lakini piya anasema kuwa kumsamehe mkosa ni muhimu zaidi.

Bi Bahrami anadai fidia kwa majaraha yake.