Kombe la Dunia 2014 makundi yapangwa

Rais wa Fifa Sepp Blatter siku ya Jumamosi ya tarehe 30 Julai, alihudhuria sherehe ya kifahari za kupanga nchi katika makundi ambazo zitakazoshiriki kuwania nafasi ya kufuzu kucheza fainali ya Kombe la Dunia zilizofanyika katika ufukwe wa pwani ya Copacabana mjini Rio nchini Brazil. Uchumi wa Brazil unakuwa kwa haraka, lakini patashika za kuelekea Kombe la Dunia hata hivyo zinaonekana kuchochea zaidi maendeleo ya uchumi.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Rais wa Fifa Sepp Blatter na Rais wa Brazil Dilma Rousseff

Hivi sasa barabara mpya zinajengwa, viwanja vya ndege navyo vinaanza kupata sura mpya inayohitajika. Kumekuwa na kuchelewa kwa hapa na pale, lakini waandalizi hivi sasa wameonesha matumaini katika kazi za maandalizi. Na tofauti na uamuzi wa kuizawadia Qatar nafasi ya kuandaa Kombe la Dunia la mwaka 2022, kwa Brazil kupata nafasi hiyo ya kuandaa, hakuna cha kutiliwa mashaka kwani kandanda ndio nyumbani kwake Brazil.

Tuangalie nchi za Afrika zilivyopangwa.

Mzunguko wa kwanza utakayo kuwa na mechi 12 za nyumbani na ugenini kati ya tarehe 11 hadi 15 mwezi wa Novemba, ambapo washindi watasonga mbele katika patashika za mzunguko wa pili.

Seychelles na Kenya

Guinea Bissau na Togo

Djibouti na Namibia

Mauritius na Liberia

Visiwa vya Comoro na Msumbiji

Equatorial Guinea na Madagascar

Somalia na Ethiopia

Lesotho na Burundi

Eritrea na Rwanda

Swaziland na jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo

Visiwa vya Sao Tome na Principe na Congo

Chad na Tanzania - - -

Kwa makundi nchi hizo zimepangwa hivi:

Kundi A

Afrika Kusini Botswana Jamhuri ya Afrika ya Kati Somalia na Ethiopia - - -

Kundi B

Tunisia, Visiwa vya Cape Verde, Sierra Leone, Equatorila Guinea na Madagascar

- - - Kundi C Ivory Coast Morocco Gambia Chad/Tanzania - - - Kundi D Ghana Zambia Sudan Lesotho/Burundi - - - Kundi E Burkina Faso Gabon Niger Sao Tome and Principe/Congo - - - Kundi F Nigeria Malawi Seychelles/ Kenya Djibouti/Namibia - - - Kundi G Egypt Guinea Zimbabwe Comoros Islands/Msumbiji - - - Kundi H Algeria Mali Benin Eritrea/ Rwanda - - - Kundi I Cameroon Libya Guinea Bissau/Togo Swaziland/Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo - - - Kundi J Senegal Uganda Angola Mauritius/Liberia

Mechi zitachezwa kati ya tarehe 1 mwezi wa Juni, 2012 na tarehe 10 mwezi wa Septemba 10, 2013.

Washindi wa kila kundi watasonga mbele hadi raundi ya tatu, wakicheza mechi za nyumbani na ugenini kati ya tareh 11 hadi 15 mwezi wa Oktoba, 2013 na washindi ndio watafuzu kucheza katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.