Itachukua miaka 30 kuisafisha Ogoniland

Image caption Mwanaharakati wa mazingira aliyenyongwa Nigeria

Eneo la Ogoniland linaweza kuchukua miaka 30 kurejea katika hali ya kawaida baada ya mafuta kuharibu mazingira, ripoti ya UN imesema.

Ripoti hiyo ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu inasema kurejesha mazingira yake ya asili kutathibisha kuwa ni eneo litakalochukua muda mrefu zaidi na kubwa zaidi kusafishwa duniani.

Ripoti hiyo imekutas kuwa athari za mazingira yanatishia afya ya jamii kwa angalau vijiji kumi katika eneo hilo.

Kampuni kubwa ya mafuta ya Shell imekiri kuhusika na matukio mawili ya kuvuja kwa mafuta yaliyoharibu mazingira katika jamii hizo mwaka 2008 na 2009.

Jamii moja ilisema itadai fidia ya mamia ya maelfu ya dola. Shell imesema italimaliza shauri hili kwa sheria za Nigeria.

Ripoti ya UN report, iliyotokna na uchunguzi wa miaka miwili, imethibitisha kuwapo kwa utata kwa sehemu kwa sababu iligharamiwa na kampuni ya Shell.

Mapema, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (Nep) liliwasilisha matokeo ya utafiti wake kwa Rais wa Goodluck Jonathan.

Nigeria ni mojawapo ya nchi zinazotoa mafuta kwa wingi duniani.

"Hii si tathmini iliyotayarishwa kulaumu mdau yeyote anayefanya kazi katika eneo la Ogoniland," Msemaji wa Unep Nick Nuttall amekiambia kipindi cha BBC cha Network Africa.

"Kile ambacho tuna matumaini nacho kwa makini ni kuwa hili litafunga ukurasa wa huzuni, hali tete na wakati mwingine habari za ghasia, zilizokuwa zikijirudia kwa miongo kadhaa.

"Tunatumaini kuwa hii itajenga aina fulani ya kushirikiana kati ya wadau mbalimbali katika eneo hili la dunia."

Mwandishi wa BBC Jonah Fisher mjini Lagos anasema tayari imejulikana kuwa ripoti hiyo inakuwa ikiangalia kisheria athari za miongo kadhaa za mafuta yaliyovuja kwa jamii za watu wanaoishi eneo la Ogoniland.

Alisisitiza pia kuwa kukubali kuwajibika kwa kampuni ya Shell kwa matukio ya kuvuja kwa mafuta mara mbili haihusiani na ripoti ya Unep.

Mafuta katika eneo la Ogoniland: Historia ya madhara

  • 1958: Mgomo wa mafuta katika Ogoniland
  • 1990: Vuguvugu la watu walioathirika Ogoni (Mosop)laundwa, likiongozwa na Ken Saro-Wiwa
  • 1993: Waogoni 300,000 waadnamana dhidi ya kutojali kwa serikali na kampuni ya Shell
  • 1993: Shell yajitoa Ogoniland baada ya mfanyakazi wake kupigwa
  • 1994: Viongozi wanne wa jumuiya ya Ogoni wauawa na kundi la vijana. viongozi wa Mosop akiwemo Ken Saro-Wiwa, wakamatwa
  • 1995: Bw Saro-Wiwa na wengine wanane wahukumiwa na kunyongwa; Dunia nzima yaishtumu serikali
  • 2003-2008: Jumuiya ya kimataifa yaelekeza macho yake kwa mgogoro wa kivita ulioanzishwa na jumuiya nyingine katika Niger Delta
  • 2011: Shell yakubali kuwa inawajibika katika matukio mawili ya kuvuja kwa mafuta katika eneo la Ogoniland spills

Martin Day, wakili anayewawakilisha watu wa Bodo katika eneo la Ogoniland, aliiambia BBC siku ya Jumatano kuwa eneo kubwa la limeharibiwa na mafuta akiimanisha kuwa jamii ya wafugaji haiwezi tena kuendesha maisha yake kama zamani.

"Matokeo yake, kwa hali hii hawawezi kuvua samaki," alisema. "Wameachwa, wengi wao, katika hali ya umaskini mkubwa."

Bw Day ameelezea kuwa uvujaji huo wa mafuta umekuwa miongoni mwa matukio yenye athari mbaya zaidi duniani lakini akasema umedharauliwa mpaka kampuni yake ilipotishia kuishtaki kampuni ya Shell katika mahakama nchini Uingereza.

Hili, alisema, litaweka mfano wa kisheria kwa jamii nyingine ambazo maisha yao yameathiriwa na makampuni ya magharibi.

Matatizo ya kimazingira yaliyosababishwa na biashara ya mafuta katika eneo Ogoniland kwanza yalianza kuzungumzwa na mwanaharakati Ken Saro-Wiwa, ambaye alinyongwa mwaka 1995 na serikali ya kijeshi ya Nigeria, na kuanzisha cheche za kimataifa kuhusu eneo hilo.

Kampeni hizo zimeilazimisha kampuni ya Shell kusimamisha shughuli za kuchimba mafuta kutoka eneo la Ogoniland lakini inaendelea kuendesha mabomba ya mafuta katika eneo hilo.

Ripoti iliyopita ya Unep iliwashutumu wenyeji wa eneo hilo kwa njama za wizi kuwa kwa 90% zimesababisha kuvuja kwa mafuta na kuleta athari na vuguvugu la wanaharakati wa eneo hilo.

Kabla ya ripoti hiyo harakati za Bw Saro-Wiwa kwa ajili ya uhai wa watu wa Ogoni (Mosop) zilishutumu hilo zikisema hawajashauriana na wenyeji vya kutosha.

Mwandishi wa BBC anasema huku SHELL ikiwa imegharamia ripoti hiyo, kutajwa popote kwa kampuni hiyo kubwa ya mafuta kwenye matokeo ya utafiti kutahitaji uchunguzi wa kina.