Suruwa zinaambukiza wakimbizi

Umoja wa Mataifa unasema uamesangazwa na ugonjwa wa surua uliozuka katika kambi ya Dollo Ado, nchini Ethiopia, ambako maelfu ya Wasomali wamepata hifadhi baada ya kukimbia ukame.

Haki miliki ya picha AP

Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, linasema ugonjwa huo ukitapakaa unaweza kusababisha vifo na maradhi makubwa, katika jamii ya wakimbizi ambao tayari ni dhaifu.

Madaktari wanasema suruwa kawaida haiui mtu mwenye afya, lakini ni hatari kwa wale wanaotapia mlo.