Mafuta yanavuja kutoka meli India

Wakuu wa India wanasema mafuta yanavuja kutoka meli iliyozama karibu na Mumbai siku chache zilizopita.

Taarifa ya Waziri wa Ulinzi, ilieleza kuwa mafuta baina ya tani moja na nusu na mbili zinavuja kila saa.

Wakuu wanajaribu kuyayusha mafuta hayo, na mashua zimeshauriwa zisivue katika eneo hilo.

Mabaharia 30 wa meli hiyo waliokolewameli ilipozama Alkhamisi.

Inafikiriwa meli hiyo, MV Rak, ilikuwa na shehena ya mafuta na dizeli zaidi ya tani mia tatu; na kuna wasiwasi kuwa shehena hiyo itachafua mazingira.