Mazungumzo madeni ya Ulaya na Marekani

Mazungumzo ya dharura yanafanywa kutwa leo, kuhusu madeni ya Ulaya na Marekani, ili kutuliza masoko ya fedha kabla hayakufunguliwa kesho.

Macho sasa yako juu ya Ulaya baada ya madeni ya Marekani kutajwa kuwa yamepungua hadhi.

Kuna wasi-wasi kuwa msuko-suko sasa utaikumba Utaliana.