Jeshi la Syria limeshambulia miji miwili

Wanaharakati wa upinzani nchini Syria wanasema jeshi la serikali limeshambulia miji miwili, na kuuwa watu kama 75.

Haki miliki ya picha DPN

38 walikufa kaskazini-mashariki katika mji wa Deir Ezzor, ambao ulianza kushambuliwa kwa mizinga alfajiri.

Waandamanaji wamekuwa wakifanya mihadhara huko tangu maandamano yalipoanza mwezi wa March, lakini taarifa za hivi punde zinasema, sehemu kubwa za mji huo, sasa zinadhibitiwa na serikali.

Wanajeshi piya wamekuwa na operesheni katika jimbo la kati, la Homs, ambako inaarifiwa watu wane wameuliwa katika mji wa Hula.