China yamtuma mjumbe wake Sudan Kusini

Sudan Huru

Waziri wa mambo ya nje wa China, Yang Jiech anaanza ziara yake ya kwanza Sudan Kusini tangu nchi hiyo kutangaza uhuru wake mwezi jana. Bw.Yang anatarajiwa kuishawishi serikali ya Juba kuimarisha uhusiano wake na Jamuhuri ya Sudan.

China imekuwa ikipokea mafuta mengi kutoka Sudan na raslimali hii imeimarisha uchumi wake unakua kwa kasi. Nyingi ya raslimali sasa imesalia Sudan Kusini japo mafuta hayo yanahitaji mabomba ya kusafirishia ambayo yanamilikiwa na Sudan.

China inahofia kwamba uhusiano mbaya kati ya Sudan Kusini na Jamuhuri ya Sudan huenda ukaathiri tegemo lake la mafuta.