Bei ya hisa yashuka tena duniani

Soko la hisa Korea Kusini Haki miliki ya picha REUTERS

Bei za hisa zimeshuka tena katika masoko ya fedha Mashariki ya Mbali kufuatia msukosuko kwenye masoko ya fedha duniani.Soko la hisa la Australia hisa zilishuka kwa pointi moja nukta sita hali sawa na hiyo ikiwa katika soko la fedha la Japan Nikkei.

Huko Hong Kong dhamani ya hisa ilishuka kwa kiwango cha chini zaidi kwa asili mia mbili.Hasara ya karibuni kwenye masoko ya fedha imechochewa na msukosuko wa uchumi wa Marekani pamoja na matatizo ya nakisi ya bajeti katika baadhi ya nchi za Ulaya.

Mwandishi wa BBC mjini New York amesema wasi wasi ulioko katika masoko miongoni mwa wawekezaji ni juu ya mstakhabali wa uchumi wa Marekani huku serikali ikitangaza kupunguza matumizi yake na kuyumbisha matumaini ya kuimarika kwa uchumi huo.