Huwezi kusikiliza tena

Ghasia za England

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema mipango ipo tayari kutumia mabomba ya maji kuwatawanya watu na polisi sasa wataungwa mkono kisheria kwa kila mbinu watakayotumia kukabiliana na waporaji na waenezaji ghasia Uingereza.

Mwandishi wetu Mariam Omar alizungumza na mwandishi na mchambuzi wa masuala ya Uingereza Suleiman Salim.

Pia alizungumza na Kebby Kitia mkazi wa Birmingham, ambapo mji huo umeshuhudia vifo vya vijana watatu.

Na alizungumza na polisi mmoja wa London ambaye hakutaka jina lake litajwe na kumuuliza sheria ya Uingereza inasemaje kuhusu jukumu lao kama Polisi