Ukuta wa Berlin unakumbukwa

Ujerumani inakumbuka ukuta wa Berlin ulioanza kujengwa siku kama leo, miaka 50 iliyopita.

Kwa miaka 28 ukuta huo ulitenganisha upande wa mashariki uliokuwa chini ya utawala wa kikoministi na ule uliokuwa sehemu ya Ujerumani Magharibi.

Siku hiyo ilikumbukwa leo kwa kusoma majina ya watu 136 wa Ujerumani Mashariki, waliouwawa walipojaribu kuparamia ukuta huo kukimbilia Ujerumani Magharibi.

Ukoministi ulipoanza kuporomoka Ulaya Mashariki, ukuta huo ulibomolewa na watu wa mji wa Berlin, mwaka wa 1989.

Katika sherehe kuu, Rais wa Ujerumani, Christian Wulff, alisema ukuta huo sasa ni historia, na Ujerumani imeungana tena kuwa taifa moja.