Kifo kwa mwanajeshi aliyestaafu Pakistan

Ramani ya Pakistan
Image caption Ramani ya Pakistan

Mahakama ya jeshi nchini Pakistan imempa hukumu ya kifo mwanajeshi aliyestaafu, baada ya kumkuta na makosa ya kujihusisha na shambulio kubwa dhidi ya makao makuu ya jeshi miaka miwili iliyopita.

Washtakiwa wengine sita, wakiwemo raia watano, pia walipatikana na hatia na walihukumiwa kifungo.

Wapiganaji waliojifunga mabomu walijaribu kuingia kwa nguvu katika makao makuu ya jeshi, mjini Rawalpindi, mwezi Oktoba mwaka 2009.

Wanajeshi 11 waliuwawa.

Tukio hilo liliripotiwa kimataifa, na lilikuwa ni aibu kwa wakuu wa usalama wa Pakistan.