Mashambulio miji ya Syria

Ramani ya Syria
Image caption Ramani ya Syria

Wanaharakati wa Syria wanasema kuwa vifaru vimeingia katika mitaa ya mji wa Latakia, Syria, wakati risasi nyingi zikisikika.

Latakia ni moja kati ya miji iliyoonesha upinzani mkubwa dhidi ya Rais Assad.

Pia kuna taarifa kuwa risasi zilifyatuliwa jana usiku katika mji wa Homs.

Wanaharakati wanasema askari wa usalama wa Syria wamewauwa watu kama 20 hapo jana.

Taarifa zinasema watu watano walikufa Douma kitongoje cha Damascus.

Televisheni ya taifa ilisema kwamba watu waliokuwa na silaha waliwapiga risasi na kuwauwa maafisa wawili wa usalama.