Cameron kupata ushauri

Ghasia Uingereza
Image caption Ghasia Uingereza

Afisa wa polisi wa zamani wa Marekani amekubali kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, mwezi ujao, ili kumshauri juu ya njia za kupambana na magenge yanayofanya uhalifu katika barabara za Uingereza; baada ya ghasia zilizotokea Uingereza juma hili.

Bill Bratton ana uzoefu mkubwa na magenge ya mitaani katika miji ya Los Angeles, New York na Boston Marekani.

Kati ya watu wataofikishwa mahakamani Uingereza leo, ni kijana wa miaka 20, aliyeshtakiwa kwa kumuibia mwanafunzi kutoka Malaysia.

Katika siku chache zilizopita mwanafunzi Ashraf Haziq amekuwa machoni mwa Waingereza hadithi yake inaonesha kuchanganya mazuri na mabaya baada ya ghasia zilizotokea Uingereza.