11 wafariki mlipuko Pakistan

Ramani ya Pakistan
Image caption Ramani ya Pakistan

Polisi kusini magharibi mwa Pakistan wamesema watu kama kumi na mmoja wamefariki baada ya bomu kulipuka kwenye mkahawa kando ya barabara.

Huenda mlipuko huo ulisibabishwa na bomu lililokuwa kwenye jengo moja huko Jaffarabad mkoa wa Baluchistan.

Kuna ripoti inayosema kuwa wakaazi wa eneo hilo walikuwa wakiwatafuta walionusurika katika miporomoko hiyo kwa kutumia mikono yao kuchimba.

Baluchistan hushuhudia mashambulio mara kwa mara ambayo yanahusika na uanamgambo.

Pia kuna wapiganajii ambao wanatekeleza shughuli zao katika eneo hilo na wana uhusiano na Taliban.