Shambulio ofisi ya Uingereza Afghanistan

Kabul
Image caption Shambulio Kabul

Washambuliaji waliojitoa mhanga wameshambulia afisi za British Council katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, na kuwaua takriban watu tisa na kushikilia eneo la afisi hizo kwa saa kadhaa.

Bomu liliotegwa ndani ya gari liliangamiza ukuta unaozingira ua na watu kadhaa waliokua wamebeba silaha nzito wakavamia sehemu za ndani.

Baada ya mapambano ya saa kadhaa Balozi wa Uingereza mjini Kabul alisema washambuliaji wote waliuwawa. .

Kundi la Taleban limesema shambulio hilo linaadhimisha uhuru wa Afghanistan kutoka Uingereza mnamo mwaka 1919.

Takriban askari polisi wanane wa Afghanistan na afisa mmoja wa usalama ambae inaarifiwa ni nimwanajeshi wa huduma maalum wa New zealand waliuwawa.

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron alilaani mashambulio hayo "ya kioga" akisema ameongea na Waziri Mkuu wa New Zealand John Key kumshukuru kwa mchango wa vikosi maalum vya nchi yake katika kulinda eneo hilo.

Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imesema raia wote wa Afrika Kusini wamepigwa na mshtuko lakini wako salama baada ya kuhamishwa kutoka jengo hilo.

Balozi wa Uingereza William Patey amesema kuna majeruhi miongoni mwa wanajeshi wa zamani waNepali wa kikosi cha Gurkha-lakini hakuna aliyekufa.