Huwezi kusikiliza tena

Viongozi Afrika wajifunze kwa Mubarak

Hosni Mubarak, akiwa madarakani kwa miaka thelathini, alikuwa kiongozi mwenye nguvu, madaraka, mamlaka kwa nchi yake ya Misri.

Bw Mubarak amekuwa akifikishwa mahakamani akiwa kwenye kitanda cha hospital kutokana na kuumwa. Kesi yake itasikilizwa tena mwezi Spetemba.

Je viongozi wa Afrika wajifunze nini kutokana na hali anayopitia kiongozi huyo aliyekuwa na nguvu na madaraka makubwa nchini mwake?

Fuatilia mjadala huu ambapo pamoja na washiriki wengine, BBC imezungumza na Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano kupata maoni yake kuhusu hilo.

Washiriki wengine ni Jenerali Ulimwengu-Mchambuzi na Mwandishi wa Habari Mwandamizi, Mgwegenzo Chovino-kutoka muungano wa vyama vya upinzani Burundi, na Ali Mutasa-mwandishi wa habari Mwandamizi.

Mjadala umeendeshwa na Zawadi Machibya.