Jeshi la Tunisia linapambana na Walibya

Wizara ya Ulinzi ya Tunisia inasema kuwa jana usiku, wanajeshi wake walipambana na watu kutoka Libya waliokuwa na silaha, kusini-magharibi mwa nchi.

Haki miliki ya picha AFP

Afisa wa wizara hiyo alisema wanajeshi waliokuwa wakipiga duru, walishambuliwa na watu waliokuwa na silaha, na waliokuwa kwenye magari yenye nambari za Libya katika eneo la Douz. Alisema Tunisia haikupata hasara yoyote, na washambuliaji hao bado wanasakwa na jeshi la wanahewa na la ardhini.

.