Mutharika afuta kazi mawaziri

Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika, amelifuta kazi baraza lake lote la mawaziri baada ya majuma kadha ya maandamano ya ghasia, ambapo watu karibu 20 wamekufa.

Haki miliki ya picha AFP

Bwana Mutharika sasa ameshika wizara zote 42; na hakutoa sababu ya kufanya hivo.

Mataifa kadha ya magharibi, yamesimamisha msaada kwa Malawi baada ya waandamanaji kuuwawa mwezi uliopita, ambao wakilalamika juu ya kupanda kwa gharama za maisha na kama walivosema, serikali mbovu.