Mapambano ya kikabila Sudan Kusini

Wakuu wa Sudan Kusini wanasema watu zaidi ya 500 wameuwawa kwenye mapigano ya kikabila katika jimbo la Jonglei, mashariki mwa nchi.

Haki miliki ya picha Reuters

Afisa wa eneo hilo (Gabriel Duot Lam) ameiambia BBC kwamba watu mia kadha wamejeruhiwa na zaidi ya 200, wengi wakiwa watoto, walitekwa nyara.

Mapigano hayo yalitokea Alkhamisi, wakati watu wa kabila la Murle inasemekana waliwashambulia Lou Nuer, na kuwaibia ng'ombe kama elfu 40.

Sudan Kusini ilipata uhuru mwezi uliopita na inakabili matatizo makubwa kuhusu usalama.