Wapiganaji wanatembea kuelekea Tripoli

Mamia ya wapiganaji wa Libya wanasonga mbele kuelekea Tripoli kutoka mji uliotekwa Jumapili, kilomita 40 nje ya mji mkuu.

Haki miliki ya picha AP

Mwandishi wa BBC anayesafiri pamoja na wapiganaji, anasema leo waliingia mji mdogo uitwao Jaddaym.

Kulikuwa na mapambano makali leo asubuhi lakini hatimaye wapiganaji waliudhibiti mji huo.

Na kutoka Jaddaym, wapiganaji hao walitembea kuelekea Tripoli.

Mwandishi wa BBC, Rupert Wingfield Hayes, anasema wapiganaji hao wanasema watafika Tripoli leo usiku.

Yeye anaona haikuelekea hivo, lakini anasema mhadhara wao unaaanza kuonekana kama mwanzo wa mhadhara wa kwenda kuiteka Tripoli.