Malema achunguzwa na polisi

Kikosi maalumu cha polisi wa Afrika Kusini, kinasema kuwa kinamchunguza kiongozi wa vijana wa chama tawala cha ANC, Julius Malema, kwa sababu ya tuhuma za ufisadi na rushwa.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Msemaji wa kikosi hicho, (kiitwacho Hawks, Mwewe) alisema uchunguzi kamili utafanywa.

Kikundi kimoja kimemripoti Bwana Malema kwa polisi, baada ya taarifa kuhusu dosari katika shughuli zake za biashara.

Amekanusha kufanya makosa.

Ijumaa, ANC ilisema kuwa inamtia adabu Bwana Malema, kwa kuchafua jina la chama.

Bwana Malema -- ambaye ametoa wito kuwa machimbo na mashamba nchini Afrika Kusini yataifishwe -- ana sauti katika ANC na anavutia watu.