Ndege za Nato zalenga handaki la Gaddafi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waasi wakijiandaa kuishambulia Sirte

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema, ndege za kijeshi za Uingereza zimerusha mabomu kwenye handaki kubwa lililopo Sirte mji alipozaliwa Kanali Muammar Gaddafi.

Ndege hizo ziliondoka kutoka kambi ya jeshi iliyopo Nolfolk siku ya Alhamis usiku.

Waasi wa Libya nao wanaimarisha majeshi yao kwenye barabara inayoelekea Sirte, wakipeleka vifaru na makombora.

Viongozi wa waasi wamezitaka serikali za kigeni kuondoa tanji kwenye mali za Libya.

Umoja wa Mataifa tayari umekubali kuachia dola za kimarekani bilioni 1.5 ya mali za Libya- ambazo zilipigwa tanji baada ya kuwekewa vizuizi - kusaidia msaada wa haraka wa kibinadamu.