Ferguson aishambulia FA

Alex Haki miliki ya picha PA
Image caption Alex Ferguson

Sir Alex Ferguson amekituhumu chama cha soka cha England FA kwa kutoipa haki Manchester United.

Meneja huyo wa United, ambaye msimu uliopita alipewa adhabu ya kukaa jukwaani katika mechi tano, ametoa tuhuma hizo wakati akizungumza kuhusiana na wachezaji wake wanane kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England.

Ferguson, 69, alisema: "FA huenda wanafahamu nani ameleta wachezaji zaidi kwa nchi yao kuliko timu yeyote ile duniani.

"Labda watafahamu umuhimu wetu kwa England kuliko kutufanya kama 'takataka'.

Matamshi ya Ferguson yamekuja wakati akizungumzia idadi ya wachezaji wake ambao huenda wakaitwa kuichezea timu ya taifa mwishoni mwa wiki.

Meneja Fabio Capello anatarajiwa kutaja kikosi chake kwa ajili ya michuano ya mwezi ujao ya kufuzu Euro 2012, dhidi ya Bulgaria na Wales. Manchester United huenda ikatoa wachezaji takriban wanane.

Ferguson amefurahishwa na hilo lakini ametumia nafasi hiyo kuishutumu FA kuhusiana na adhabu ilizopewa klabu hiyo msimu uliopita.

"Nafurahia wachezaji wangu, ni wazuri."

FA imegoma kuzungumzia tuhuma za Ferguson.